GET /api/v0.1/hansard/entries/1402643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1402643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402643/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwenye kamati hiyo, kulikuwa na Wakili Fatuma Dullo, Wakili Amos Wako, Wakili Okong’o Omogeni, Wakili Orengo, mimi na wengine. Tulimpa mikoba ambayo anaendelea kuitumia hadi sasa. Kwa hivyo, hawezi kukosea. Vile vile, ningependa nimpongeze kwa kauli aliyotoa jana kuhusiana na jumba la Bunge Tower. Bw. Spika wa Muda, kuna wabunge zaidi ya 400. Wengine watachukuwa ofisi pale kwa kuwa usalama wao ni muhimu sana. Tukija katika Mswada huu, naunga mkono kuwekwa kwa threshold ya thuluthi mbili iwapo unataka kumuondoa mamlakani waziri katika kaunti zetu. Tumeona kwamba mawaziri katika kaunti zetu hawajakuwa na msisimko wa kisawasawa kwa sababu mara nyingi, wanaangalia gavana anafanya nini. Wanapokuwa karibu sana na gavana, Wabunge wa Bunge la Gatuzi wanachukulia kuwa ni unyonge kisha kuwatoa mamlakani kiholela. Hii sheria itasaidia pakubwa kuweza kuleta haki katika wale wanaotaka kuondolewa katika mamlaka ya uwaziri katika kaunti zetu. Bw. Spika wa Muda, tumeona kwamba mara nyingi magavana wanakaba sana kutoa mamlaka kamili kwa waziri. Utapata kwamba waziri mara nyingi anaangalia gavana anasema nini ndiposa afanye kazi. Wanapochaguliwa wanaapishwa kwamba watafanya kazi kulingana na sheria na katiba ya Kenya."
}