GET /api/v0.1/hansard/entries/1402648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1402648,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402648/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, tunasema kwamba ni swala muhimu kuwe na mamlaka ya kuhakikisha kwamba wale wanaoondolewa mamlakani wanatendewa haki. Kumuondoa mtu mamlakani kama alivyoondolewa naibu gavana wa Kisii mwezi uliokwisha ni jambo nzito sana kisheria kwa sababu unamfunga yule mtu kutofanya mambo ya kisiasa na pia kupata kazi serikalini inakuwa ni shida. Kwa hivyo, lazima kuwe na kiwango fulani ambacho kikifikiwa mtu yule anaweza kutoka kwenye mamlaka. Mengi yamezungumzwa kuhusiana na maswala ya kuondoa mamlakani viongozi. Sisi kama Bunge la Seneti tuna mamlaka ya kumuondoa hata Rais. Ila cha kusikitisha, hatuna mamlaka ya kumuondoa waziri katika serikali kuu. Tuliona hapa kwamba kuna mawaziri ambao wana utepetevu mwingi katika kuendesha kazi zao, ila hatuna mamlaka ya kuwaondoa. Naibu wa Kiranja wa Upinzani, Seneta Sifuna, alileta Hoja ya kumcensure Naibu wa Rais lakini haikuona mwangaza. Sina neno la Kiswahili ambalo naweza kutumia kwa sasa ndio maana nikatumia censure ."
}