GET /api/v0.1/hansard/entries/1403158/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403158,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403158/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Hoja hii. Kabla sijaanza, naungana na Taifa la Kenya na Wajumbe wenzangu hata nimuomboleze shujaa Generali Ogolla ambaye tulimpoteza. Natoa rambirambi zangu binafsi na za watu wa Taita Taveta kwa familia ya Generali na Taifa lote la Kenya na majeshi yote ya nchi hii. Nasema pole. nGenerali Ogolla ameombolezwa kama mweledi katika kazi yake. Vile vile, alikuwa kipenzi cha wengi; wakubwa kwa wadogo, maskini kwa tajiri, na watoto kwa wazee. Pole sana kwa wote wanaoomboleza."
}