GET /api/v0.1/hansard/entries/1403209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1403209,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403209/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Turkana West, UDA",
"speaker_title": "Hon. Daniel Nanok",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nami niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa jamii ya Jenerali Ogolla pamoja na maafisa waliofariki katika ajali ya ndege iliyotokea kwenye Kaunti za Elgeyo Marakwet na West Pokot. Imekuwa huzuni kubwa nchini kwa sababu mmoja wa waliofariki alikuwa kiongozi mkuu wa Jeshi letu la Kenya. Na mambo kama hayo yanapotokea, yanatukumbusha mambo mengi kuhusiana na wanajeshi wetu. Ndiyo maana tunaweza kuongelea mambo ya askari wetu na namna wanavyoshughulikiwa katika nyanja tofauti humu nchini na kule nje."
}