GET /api/v0.1/hansard/entries/1403245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403245/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, nampongeza Mjumbe wa Lamu Mashariki kwa kuleta Hoja hii. Anataka maafisa wa jeshi wapewe heshima zao. Ameleta Hoja hii kwa sababu ya mchakato unaoendelea katika eneo bunge lake. Pale ni karibu na msitu wa Boni. Anawaona wanajeshi wakihangaika na hawalali. Wakati wa mafuriko, wanaishi katika mashimo yaliyo na maji, wakishika doria kuhakikisha kwamba adui haingii kwetu. Kwa hivyo, kuwapatia heshima wanajeshi ni vyema zaidi. Ni watu wanaojitolea kukaa mbali na familia na watoto wao. Wanarudi baada ya mwezi mmoja au miwili. Kwa hivyo, ni vyema sana wapewe heshima zao."
}