GET /api/v0.1/hansard/entries/1403248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1403248,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403248/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "tunalindwa. Hatuwezi kuwa na maendeleo kama hatuna ulinzi wa nje. Lakini, kuna vikosi vya ulinzi wa ndani ambavyo havilali. Nilifanya kazi katika kikosi cha General Service Unit (GSU) miaka tisa. Najua kazi ngumu wanayofanya. Wanaishi msituni mpaka wanafanana na nugu. Kuna wakati tulikuwa Chepchoina tukipambana na wezi wa mifugo. Kukatokea shida Mount Elgon kule juu na sisi tulikuwa katikati. Tulisikia kelele za wananchi kule juu. Ikabidi twende kule juu. Wale majambazi walikuwa wanarusha risasi kuja chini - risasi ambazo zilikuwa zinawaka moto. Lakini, tulienda kuokoa maisha. Kwa hivyo, hata vikosi vyetu vya usalama wa ndani vinapata shida sana. Ni vizuri waingizwe katika hiyo kombo wapatiwe heshima zao. Naona muda wangu unaisha. Huduma za afya kwa askari ni muhimu sana. Askari wengi wakistaafu wanakuwa wagonjwa sana. Hawawezi kupata matibabu kwa sababu hawapati fedha za kutosha. Kwa vile walifanya kazi katika vikosi vya ulinzi wa usalama wa ndani na nje, hata kama wamestaafu, wapatiwe huduma ya afya kwa sababu wengi wao huwa ni wagonjwa. Nimepiga attention miaka tisa mpaka nasikia kiuno kina taabu, lakini inabidi nijitibu mwenyewe. Serikali inafaa kuchukua jukumu hili. Hawa watu wana familia. Watu wengi katika familia zao wanarandaranda na hawasomi maafisa wa polisi wanapostaafu. Tuwasaidieni."
}