GET /api/v0.1/hansard/entries/1403264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1403264,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403264/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": "ni ndugu zetu, tunaishi nao, na tunajua kazi wanayoifanya ni ya kujitolea lakini mishahara yao ni duni sana. Pindi wanapostaafu, mara nyingi maisha yao huwa duni kwa sababu ya yale mapato waliyokuwa wakipata walipokuwa wakihudumia taifa hili. Nimekutana na wanajeshi wengi sana ambao wanaishi maisha ya uchochole. Miaka imesonga na hawawezi kufanya kazi yoyote. Wengine wameshastaafu kutoka kwa jeshi lakini wanatafuta vibarua katika hoteli kule Pwani. Unapata bado wanatafuta vibarua kama security officer katika hoteli. Ni jambo la aibu. Tungependa wakistaafu waishi maisha mazuri na watoto wao. Watoto wao pia wapate elimu na maisha yaendelee vizuri. Hakuna watu wengine watakaowatetea isipokua Bunge hili. Kwa hivyo, lazima tudumishe na tungeneze sheria maalum ya kuwalinda ndugu zetu wanajeshi. Naiunga mkono Hoja hii iliyo mbele ya Bunge hii iliyoletwa na dadangu, Captain Mhe. Ruweida, Mbunge wa Lamu Mashariki."
}