GET /api/v0.1/hansard/entries/1403439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403439,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403439/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "nyingi. Ni vizuri kuwe na maelezo kamili ni kwa nini Mdhibiti wa Bajeti anapitisha pesa zilipwe kwa malipo aina fulani lakini hayo malipo yanasimamishwa na malipo yanaenda kwa kazi tofauti. Hili pia limepelekea kuongezeka kwa bili zilizosalia. Hii inaoenyesha ya kwamba hakuna huduma zitatolewa katika kaunti zetu. Hivyo basi, hili ni swala la kulivalia njuga. Hili ni swala ambalo kama Seneti, tunatakikana tusimamishe kazi zote ili kuangazia njia tutakayo tumia kuhakikisha ya kwamba pesa zinazopatikana kwa kaunti zinatumika kulipa bili zilizosalia. Na kwamba, zile kaunti ambazo hazitalipa bili zilizosalia kulingana na Kanuni 50(2) (3) ya Public Finance Management Act Regulations, kuwe na adhabu ya kutosha. Jambo lingine ambalo linapelekea kulimbikiza kwa bili zilizosalia ni bajeti ya ziada. Wakati tunatengeneza bajeti katika mwaka wa pesa, kuna pesa zinazotengwa za miradi kadha wa kadha. Kutengeneza bajeti kunatumia uhusishaji wa wananchi. Wanajua ni miradi gani wanataka ifanyike. Lakini, inafikia mahali kuna kuwa na bajeti za ziada ambazo zinatoa miradi yao. Wananchi hawaelewi ni kwa nini miradi yao haijafanyika. Mara nyingine, Maseneta wanalaumiwa ya kwamba pesa zinaibwa na hawasemi jambo lolote. Kwa sababu mradi wa wadi fulani ulikuwa katika bajeti lakini mwaka umeisha na ule mradi haujafanyika. Maseneta wanaendele kulaumiwa ya kwamba pesa zinaibwa na hawapigi kelele. Kumbe kuna bajeti ya ziada imefanyika ambayo haijahusisha mwananchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}