GET /api/v0.1/hansard/entries/1403440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403440,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403440/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Kwa hivyo, hii Hoja inasema ya kwamba wakati bajeti ya ziada inapo tengenezwa, ni vizuri kuwe na uhusishaji wa jamii na wananchi wajue sababu za kuondoa mradi katika bajeti. Bw. Spika, la mwisho, wakati wa bajeti ya ziada, kama haijahusisha mwananchi, basi Mdhibiti wa Bajeti asipitishe hiyo bajeti. Nimeona kama kwetu Taita Taveta, wakati wa kuandaa bajeti ya ziada ambayo nafikiri ni ya tatu huu mwaka, pesa za wadi zilikuwa shilingi milioni ishirini. Lakini, zimepunguwa kwa kiasi cha shilingi milioni nane na zikabakia shilingi milioni kumi na mbili. Wananchi hawajui kama kama shilingi milioni nane zimetolewa zikaenda kujenga Aggregation Centre ama industrial park ambayo wao wenyewe hawajahusishwa. Nafikiri inatakikana tuchambue maandalizi ya bajeti kama Seneti. Hii ndio kazi ya Seneti ya ndani zaidi ambayo inatakikana ipatie kaunti zetu na wananchi meno ya kuhakikisha kwamba zile pesa wanapata kama ushuru zinatumika vile zilivyo pangiwa. La sivyo, tutakuwa tunapata malimbikizi ya bili zilizosalia, miradi haifanyiki na hatuelewi ni kwa nini, kumbe imetolewa kwa sababu ya bajeti ya ziada ambayo wananchi hawahusishwi na maandalizi yake. Hayo malimbikizi ya bili zilizosalia yanatakikana pia yaharamishwe na watu wafungwe. Singependa kuongea zaidi ya hapo. Ninaunga mkono hii Hoja iliyoletwa na Sen. Olekina. Ningerai wenzangu wapitishe Hoja tuangalie utekelezaji wa hayo mapendekezo ambayo yatapelekea kusaidia wananchi wetu wanaofanya kandarasi na serikali za kaunti. Hii italeta maendeleo, huduma na miradi ifanyike vizuri. Nashukuru sana kwa hii nafasi."
}