GET /api/v0.1/hansard/entries/1403500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403500,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403500/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "katika kaunti ya Marsabit, ambayo nasimamia kama Seneta, ambao kulingana na ofisi ya CoB, wamelipwa. Nimepewa hizo documents kutoka kwa hiyo Ofisi na wale contractors wangefaa kulipwa, walisema hawajapata hiyo pesa nilipowauliza. Bw. Naibu Spika, sababu nyingine inayofanya pesa ya contractors na suppliers kucheleweshwa ni Own Source Revenue (OSR); ule ushuru unaonafaa kukusanywa katika kaunti. Wakati bajeti inapangwa, wanaongeza kiwango ambacho wanafaa kuokota kiwe zaidi. Hiyo inafanya suppliers wa kaunti wakose. Bw. Naibu wa Spika, shida ya tatu ni wakati bajeti imepitishwa na ushirika wa umma umefanywa, kuna kitu kinachosumbua sana ambacho kinaitwa supplementarybudget. Kwa mfano, baada ya bajeti kupitishwa kwa kaunti yangu ya Marsabit, yale maendeleo yangefanywa kama ujenzi wa barabara, nyumba, mashule au mahospitali na yalikuwa kwa bajeti, yale yaliyopangwa yanabadilishwa na supplementary budget inatengenezwa. Pesa zote zinatolewa kwa hayo maendeleo na zinapelekwa kwa"
}