GET /api/v0.1/hansard/entries/1403507/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403507,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403507/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, mwenzangu ameteleza kidogo. Sijasema iko dini inaonyesha mwingine ni mkora. Lakini, ninasema wale watu tungeheshimu kama Waisilamu, wanatoa sadaka na wanaenda Hajj, wangefaa kuhakikisha kaunti zao zinafanya kazi vilivyo. Ugatuzi unakufa. Nilienda manyatta fulani. Nikaonyeshwa kaburi na nikaambiwa huyu mzee amekufa akidai kaunti. Kuna watu wengi sana wamepotesha maisha yao na siyo kwa sababu ya ugonjwa au shida nyingine. Ni kwa sababu alienda kuomba pesa kwa benki, familia au marafiki zake ili aende kufanya kazi ya kaunti. Bw. Naibu wa Spika, pesa inakaa miaka tano bila kutolewa au kulipwa. Ninakubaliana na Sen. Olekina. Ningeulizwa leo, maendeleo yoyote yale yasifanywe ili kwanza walipe zile pesa zote au pending bills watu wanadai serikali za kaunti na Serikali Kuu. Haijalishi serikali ni gani. Kama ni ya kaunti am ani Serikali Kuu ya Kenya. Saa hizi ukipatikana na Kenya Revenue Authority (KRA) na hujalipa ushuru, unapigwa penalty. Sasa, Serikali inakupiga penalty na wakati ule Serikali inakataa kulipa raia pesa zao, watalipa hio penalty kutoka wapi na watauliza nani? Mahali nimetoka, umaskini wa watu uko hali ya juu. Saa hizi kazi yeyote inayofanywa katika Kaunti ya Marsabit, wale wenyeji huko nyumbani hawafanyi hiyo kazi. Ni watu kutoka nje wanakuja kufanya kazi na saa zingine wanaleta chakula ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}