GET /api/v0.1/hansard/entries/1403557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403557,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403557/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Nilikuwa na swali kuhusu wafanyikazi wa maktaba. Kabla ya huduma za maktaba kugatuliwa, kuna pesa zilizotolewa za kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa maktaba. Pesa hizo hazikutumika kuwapandisha vyeo na kubadilisha mishahara ya watu wanaofanya kazi katika maktaba. Wale wafanyikazi waligatuliwa wakati maktaba ziligatuliwa, pesa iliyotengwa haikutumika kuwapandisha vyeo. Swali langu ni, je, sijui kama mkurugenzi wa maktaba yuko hapo - hawa wafanyikazi watapata pesa zao? Watapandishwa vyeo? Wengi wao wamefanya kazi kwa miaka 15 bila kupandishwa vyeo. Wakati wao wakupandishwa vyeo ulipofika maktaba yaligatuliwa na pesa ziliyotengwa hazieleweki zilipoenda. Niko na Kauli ambayo niliwasilisha hapa Bungeni lakini sijapata jibu. Waziri anaweza kuchukua fursa hii kulijibu swali hili."
}