GET /api/v0.1/hansard/entries/1403567/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1403567,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1403567/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, wanasema kuwa, mgala muue na haki umpe. Nimefurahia sana kusikia Waziri mmoja wa Serikali hii akikiri kwamba kuna mambo ambayo ni ya ugatuzi na Serikali Kuu haifai kuhusika na masuala yale haihusu Serikali Kuu. Ni Waziri wa kwanza katika Serikali hii ya Kenya Kwanza ambaye nimesikia akisema hayo. Imenishangaza kwa njia nzuri kwani mara nyingi kunaletwa Miswada hapa Bungeni ambayo siyo kazi ya Serikali Kuu. Hata hivyo, pale mwisho amejikanganya. Kama ni kweli hizi libraries zimegatuliwa ama zinafaa kusimamiwa na serikali za kaunti, library ambayo iko kwenye Kaunti ya Nairobi pale Upper Hill inafaa kuwa ikisimamiwa na Kaunti. Jibu ambalo Mhe. Waziri amelitoa halijaniridhisha. Alivyosema kuwa kunahitaji pahali pa kuweka stakabadhi muhimu za serikali ambazo ni za kihistoria, ndio maana tuna ile National Archives ili kuweka zile stakabadhi za serikali ambazo zinaweza tumika kama references wakati ambapo masuala ya kitaifa yanajadiliwa. Mimi bado sijaridhika. Jinsi ambavyo Waziri amekiri kwamba huduma za maktaba zimegatuliwa, ile maktaba iliyoko Upper Hill iwekwe chini ya Kaunti ya Nairobi. Kama anaamini kile anachosema atuhakikishie na ahakikishie watu wa Nairobi kwamba wiki hii maktaba ile itawekwa kwenye mikono ya serikali ya Kaunti ya Nairobi. Bw. Naibu Spika, nashukuru."
}