GET /api/v0.1/hansard/entries/1404247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404247,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404247/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa na mimi nipenyeze sauti yangu kusema pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia za wanajeshi waliopoteza maisha yao siku ya Alhamisi. Sisi, kama Eneo Bunge la Kisauni, tumempoteza Brigadier Swale Saidi. Alikuwa kijana shupavu mwenye mategemeo yake makubwa kwamba huko mbeleni, angechukua nafasi kubwa katika familia ya jeshi. Lakini kila kitu ni mpango wa Mungu. Kikubwa tunasema tunawaombea Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, na awasamehe dhambi zao. Ni vyema sana pia sisi, kama taifa, tufanye uchunguzi wa kina ili kujua sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo. Hii ni kwa sababu ikiwa ndege ambayo imebeba Mkuu wa Majeshi inaweza kuanguka kiholela, basi ni hatari kubwa sana kwa hizi ndege zetu ambazo zimebaki. Niko na imani kwamba ndege anayotumia Mkuu wa Majeshi na wale anaofuatana nao lazima iwe imechunguzwa kwamba inaweza kupita hata hali ya anga ikibadilika. Lakini kama inaweza kuanguka, basi inamaanisha kwamba ndege zetu zote ziko katika hatari na wasiwasi. Nchi nyingi zimetushangaa kwamba sisi tunapoteza Jenerali kwa ajali ya ndege, na hakukuwa hata na ndege ya kumsaidia. Hakukuwa na reinforcement ya kumfuata kwa karibu ili itoe msaada kwa hali kama hiyo. Ndege hiyo ilipoanguka, basi ikawa hivyo. Kwa hivyo, ninasema pole ndugu na familia. Tunawaombea Mungu awalaze mahali pema na awasamehe dhambi zao. Ahsante sana."
}