GET /api/v0.1/hansard/entries/1404301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404301,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404301/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Migori County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Nakushukuru Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Sisi kama Waislamu kawaida tumejitayarisha kufa. Tunajua kufa ni haki ambayo mtu hawezi kuchelewesha wala kubadilisha. Lakini tunahuzuni kama watu wa Nyanza. Huyo alikuwa kijana wetu ambaye tulipeana kwa nchi na tumekubali amekufa. Ila nashangaa, maanake kila mtu ambaye ameongea hapa, analaumu kwamba ndege ilikuwa na hitilafu. Mumejuaje ndege ilikuwa na hitilafu? Mimi kama Mkenya nawaomba muwe na utulivu kwa sababu tunachangia kifo cha mtu aliyekuwa wa maana sana na tunahuzunika. Naomba muwapatie wanaofanya uchunguzi nafasi nzuri yakutuambia nini iliua Generali. Kama wanajua ndege ilikuwa na hitilafu basi wachukue lawama kwa sababu inaonekana tayari nini kilitendeka. Zaidi, naomba Serikali ipeane pole kwa familia ya Generali Ogolla ambaye amelaumiwa kisiasa. Tutakuwa tunafanya utani tukisema tunahurumia familia yake na huku tunamlaumu kisiasa ila hakuwa anafanya siasa. Tafadhali tupatie familia na Wakenya waliokuwa wanampenda nafasi ya kuomboleza. Tuwachie Serikali na wale ambao wanafanya uchunguzi nafasi ili tujue kile kilichomuua. Kama ni ajali tujue ni ya aina gani na ilifanyikaje na kwa sababu gani. Tujue hitilafu ilikuwa wapi. Lakini tusipeane jibu kabla hatujajua nini kilifanyika. Naomba Mwenyezi Mungu…"
}