GET /api/v0.1/hansard/entries/1404441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404441/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu wa Tume ya Ardhi tukizingatia ya kwamba Wakenya walipiga kura ya kubadilisha Katiba. Mojawapo ya mabadiliko ilikuwa kuunda Tume ya Ardhi. Sababu ya kuunda Tume ya Ardhi ni kuwa kulikuwa na malalamiko mengi sana kuhusu dhuluma za kihistoria za ardhi. Kifungu 62 cha Katiba kinasema kuwa ardhi ya umma itakuwa chini ya usimamizi wa Rais kupitia Tume ya Ardhi. Hivyo basi, Tume hii ni muhimu sana. Kifungu 67 kimezungumzia kuanzishwa kwa Tume ya Ardhi na majukumu yake, ikiwemo usimamizi wa ardhi za umma. Kati ya majukumu hayo, kuna kusimamia ruzuku. Kwa wale ambao hawataelewa, ruzuku ni grants . Kwa hivyo kuna suala la kuzisimamia na kutathmini kama ugavi wake ulikuwa sawa ama ulikuwa na shida. Muda ambao ulipatiwa Tume ya Ardhi kuangalia masuala haya ulikuwa miaka mitano. Sasa hivi, tunachelea ya kwamba Tume itakosa mamlaka hayo. Lakini bado tuko na matatizo nyeti sana haswa mambo ya dhuluma inayotokana na ardhi. Machafuko mengi sana katika taifa letu la Kenya yalikuwa kwa sababu ya shida zilizotokana na umilikaji wa ardhi. Hii ndiyo sababu tulisema tuwe na Tume itakayosaidiana na Wizara ya Ardhi katika kutathmini suala hili la matatizo ya ardhi na kuangalia ruzuku. Katika sehemu nyingi za taifa la Kenya, kuna watu ambao walipatiwa ruzuku kwa njia za kisiasa na ambazo hazikuwa mwafaka wala sawa. Katika ardhi zile, watu hawapatikani, hawaonekani na hawajulikani wako wapi. Wakati Serikali inajaribu kutatua matatizo ya maskwota kwa kutumia ardhi kama hizi, inakuwa ni shida kwa sababu wale waliopatiwa hawapatikani. Lazima Tume ya Ardhi iendelee na kazi yake ili tuweze kuangalia ruzuku hizi zilipeanwa kwa njia gani. Je, wale waliopatiwa ruzuku hizi bado wako ama hawako? Na kweli The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}