GET /api/v0.1/hansard/entries/1404445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404445,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404445/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Nilikuwa katika Kamati ya Ardhi katika Bunge lililopita. Najua, hadi sasa, kesi ambazo bado hazijaamuliwa ili kuwasaidia Wakenya ni nyingi mno. Hata tukitathmini hali hivi sasa tuchunguze Tume imetufanyia kazi ngapi katika kutatua dhuluma za kihistoria za ardhi na kutatua mambo ya ruzuku, tutapata kwamba bado shida ni nyingi na bado hatujapata uamuzi wowote. Tusianze kuvunja nguvu ama zile Tume ambazo sisi wenyewe tuliunda kupitia Katiba ya mwananchi. Tulisema kwamba Wanjiku aliongea, Kadzo ameongea, na Achieng’ ameongea. Kwa hivyo, waliongea kwa sababu za kimsingi, haswa kuhusu suala la ardhi. Mhe. Naibu Spika, suala la ardhi limeleta maafa katika taifa letu la Kenya. Limeleta sintofahamu katika jamii, haswa ardhi za umma. Hizo siku za nyuma, watu hawakuwa na uwezo wa kutengeneza stakabadhi ama kuziweka katika njia ya kisheria. Watu walikuwa wanajua ardhi ya jamii fulani, ni ardhi yao. Hivyo basi, wale wezi wa mashamba waliweza kufanya mambo ambayo si halali na kupata umiliki wa mashamba ya umma ambayo si mashamba yao. Ni lazima tupatie Tume ya Ardhi nafasi mwafaka na ya kutosha ili Wakenya na jamii zote katika ardhi zetu za umma wapate haki. Iwapo hawatapata haki itakuwa kwamba fedha iliyotumika kubadilisha Katiba ama kuunda Tume imetumika kufanya kazi bure. Zile fedha za ushuru za mwananchi wa Kenya zitakuwa zimeenda pasi na kuwa na faida. Hili ni suala nyeti na lazima tulipatie kipaumbele kwa sababu Katiba yenyewe ishalizungumzia. Kama viongozi wa Bunge, hakuna ambaye hajaletewa matatizo ya ardhi ya dhuluma za kihistoria katika eneo Bunge lake. Tuna matatizo haya kila mahali. Kuna yale maeneo tunajua yalikuwa na matatizo sana, kwa mfano, Bonde la Ufa na ukanda wa Pwani. Jumla, Kenya nzima imekuwa na shida kuhusu ardhi.Tukisema kwamba hili suala tunaliacha, itabidi tuanze tena kutafuta sheria nyingine, kwa mfano, kurudisha jambo hili katika Wizara ya Ardhi ama tutengeneze taratibu nyingine za kusimamia suala hili. Kwa nini turudi nyuma wakati tulikuwa tushaenda hatua fulani ya kuweza kutathmini swala kama hili la dhulma ya kihistoria na kuweza kuzungumzia mambo ya ruzuku?"
}