GET /api/v0.1/hansard/entries/1404451/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404451,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404451/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuzungumzia swala la National Land Commission . Ni vizuri sana kwa kitengo hiki. Katika taifa la Kenya, tatizo kubwa linalolikumba ni swala la ardhi. Na wao haswa walikuwa wamekuja kwa sababu ya kutatua uzito au matatizo ya ardhi yaliyotokea kwa kipindi cha nyuma. Kikubwa ni kwamba ningeomba wapewe nguvu zaidi ili kusudi wawe wanaweza kutatua matatizo. Sio kusikiza halafu wanawacha. Kuna ardhi nyingi ambazo wenyewe hawako, wako Oman, sehemu za bara la Waarabu, wengine wako Ulaya, lakini ardhi zile ziko hapa na watu bado wanaambiwa ni maskwota. Mtu anakuja tu na kusema nimepewa kibali na korti kusimamia mtu lakini yule mtu mwenye ardhi halipi kodi ya kaunti wala chochote. Hii tume ya ardhi ipewe nguvu ili ikigundua kwamba hii ardhi mwenyewe hayuko, wale wanaoishi pale waweze kugawanyiwa. Wengi wamelia kwa matatizo ya ardhi. Wamejenga nyumba, wamekaa kwa kipindi kirefu, halafu inatokea ghafla wanakuja na kuwavunjia majumba yao. Hii Tume ya Ardhi ya Kitaifa izidi kupewa nguvu kisheria ili wakati wanapogundua kwamba hili jambo kweli limefanyiwa katika dhulma ya kihistoria, waweze kuwagawanyia wale walioko pale. Pwani nzima kulitokea historia ambazo ni za kidhulma. Hata kule juu upande wa bara wana shida kama hiyo. Kwa hivyo, nimesimama pia kupongeza na kuunga mkono tume hii izidi kupewa nguvu na uwezo wa kuweza kutatua matatizo. Naunga mkono. Asante sana Mhe. Naibu Spika."
}