GET /api/v0.1/hansard/entries/1404453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404453,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404453/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi niweze kuunga mkono marekebisho ya sheria ya Tume ya Ardhi. Swala la ardhi ni nyeti ambalo limetoa tumbo joto katika nchi yetu. Pwani imeathirika sana na mambo ya mashamba. Watu wengi wameitwa maskwota katika ardhi ambayo wamezaliwa na kukaa kwa miaka zaidi ya hamsini. Eneo langu la Bunge la Kaloleni halijasazwa. Katika sehemu za Shangia na Barracks, watu walikuja wakatolewa na kupelekwa mahali kwingine. Kufika kule, ile ardhi walioahidiwa wakaambiwa hakuna, wakarudi pale. Tume ya Ardhi ndio ilikuwa tegemeo la Wakenya ambao wamepoteza mashamba yao. Tunataka kuipatia nguvu, kuwe na muda wa wao kufanya uchunguzi wa dhulma za mashamba. Iweze kupatiwa muda wa kuchunguza. Inapobainika kwamba watu walidhulumiwa, waweze kurejeshewa ardhi yao. Mhe. Naibu Spika, ni jambo la kutamausha kwamba siku hizi mabwenyenye ambao wamekuwa wakichukua ardhi za watu wachochole ambao hawawezi kuenda mahakamani kujitetea, wametumia mahakama kama njia moja ya wao kujipatia ardhi kinyume cha sheria. Kumekuwa na uvunjaji wa manyumba. Inawezekanaje mtu ameketi kwa ardhi, amejenga nyumba yake, ameishi na familia yake kwa muda wa miaka ishirini, thelathini au hamsini na hakuna mtu anayesema hii ardhi ni yangu, halafu mtu anatokea mahali akisema ana stakabadhi? Kumekuwa na utepetevu katika idara ya ardhi. Tunataka hii Tume ya Ardhi iweze kuhakikisha kwamba inafanya haki. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}