GET /api/v0.1/hansard/entries/1404456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404456,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404456/?format=api",
    "text_counter": 240,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": "awamu ya kwanza ianze, kuna watu hadi leo hawajalipwa fidia. Ukiangalia pesa zao ni kidogo. Wale matajiri ambao walikuwa katika ardhi hizo wote walilipwa. Kuna utepetevu ndani ya Tume ya Ardhi. Tunataka kuwapa nguvu lakini pia watendee wale Wakenya wanyonge haki. Wakiwa watafanya uchunguzi, tunataka tume ya ardhi iweze kusajili zile kesi zote ambazo watakuwa wamepatiwa na wananchi katika gazeti rasmi la serikali ili tujue ni ardhi gani na sehemu gani ambao wanafanya uchunguzi. Uchunguzi ukiisha, tunataka wakitoa maoni yao, yazingatiwe na yapelekwe kwenye mahakama. Ndio ipitishwe na mahakama kwamba ardhi ile iweze kurejeshewa wenyewe. Tume ya Ardhi ikishirikiana na wizara wanaweza kutatua taabu za ardhi hapa nchini. Lakini shida ni maafisa ambao wako ndani ya Tume ya Ardhi na wengine wako katika wizara. Wanagandamiza na kuwadhulumu wananchi wadogo ambao kule mashinani hawawezi kutoa pesa ya hatimiliki zao. Ninaunga mkono urekebishaji wa sheria hii kusema kwamba tume ya ardhi ipewe muda wa kuweza kuchunguza dhulma za kihistoria za ardhi. Lakini pia nao wawe wazi kuhakikisha wanatendea haki nchi hii kwa kuhakikisha kwamba wale wanyonge ambao ardhi zao zimechukuliwa kimakosa ziweze kurejeshwa. Asante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa wakati huu. Asante Mhe. Owen kwa kuhakikisha kwamba umeleta Mswada huu wa kufanya marekebisho kwa Tume ya Ardhi."
}