GET /api/v0.1/hansard/entries/1404496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404496,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404496/?format=api",
    "text_counter": 280,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Wale walio na mashamba makubwa na hawayafanyi chochote, hawazalishi chakula, hawapati watu wafanye biashara, waweze kutozwa ushuru mwingi ili waweze kutumia mashamba yale. Maanake wengi wameyashikilia tu na baadaye wanauza na kupata pesa nyingi na pia wanakosa kuchangia katika kikapu cha Serikali cha mapato. Mhe. Naibu Spika, kuna mashamba matatu ambayo yanatusumbua sana pale kwetu Taita Taveta. Kando na kusumbua, wananchi wanalalamika sana maanake mpaka leo hatuna uhakika mashamba yale yalichukuliwa vipi na kama wale ambao wanayamiliki wanayatumia vipi. Kuna shamba pale kwangu Wundanyi linaloitwa Kedai Estate ambalo lilikua shamba la makonge miaka iliyopita na limekaa bila kutumika kwa muda mrefu. Shamba lile linasemekana kwamba liliuzwa. Ni shamba la ekari 10,000 na shambani mle tayari shule zimejengwa. Kuna shule mbili ndani. Kuna watu karibu 6,000 lakini kila mara wananchi wakiwa pale wana wasiwasi kwamba watafurushwa. Shamba lingine ambalo leo limeleta tumbo joto kule Taita Taveta ni shamba la makonge linaloitwa Taita Estate. Mhe. Spika wa Muda, wenye shamba lile wako na hatimiliki za kuonyesha kuwa walinunua shamba hilo lakini bado wananchi wanalalamika sana kwa sababu makonge yamepandwa kwenye ekari 33 kule Mwatate. Imefika kipindi sasa wenyewe wamekata ekari 3,000 ambazo wanataka kuwauzia wananchi. Lakini wananchi hawaelewi kwa nini shamba lile lilichukuliwa kutoka kwa wananchi wa Taita Taveta. Ni vipi leo litauziwa watu wale wale wa Taita Taveta? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}