GET /api/v0.1/hansard/entries/1404956/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404956,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404956/?format=api",
"text_counter": 332,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii. Kabla sijaendelea na Hoja hii, ningependa kuwaomba radhi baadhi ya Maseneta ambao walitarajia kwamba tutaizungumzia Hoja hii kwa lugha ya Kingereza. Ijapokuwa awali nilileta Hoja kwa lugha ya Kiingereza, nimeona itakuwa bora tuizungumze kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi nchini waweze kufuata, hasa watu wa Kaunti ya Mombasa, waweze kuelewa yale tunayo zungumzia. Hoja ni kuidhinishwa kwa ruzuku ya masharti kwa ujenzi wa uwanja wa Munisipaa ya Mombasa. KUFAHAMU KWAMBA sehemu ya pili ya Ratiba ya nne ya Katiba ya Kenya, inazipa serikali za kaunti jukumu la kuanzisha, kuendeleza, kusimamia, na kudumisha vifaa vya michezo na kitamaduni ambavyo ni pamoja na viwanja vya michezo, vituo vya utamaduni, na miundombinu mingine inayohusiana; IKIKUMBUKWA kuwa ukanda mzima wa Pwani nchini hauna uwanja wa kisasa, uliojengwa kwa viwango vya kimataifa hivyo kuwanyima wananchi manufaa yanayotokana na viwanja na vifaa kama hivyo; WASIWASI kwamba ujenzi wa uwanja wa michezo ya Manisipaa ya Mombasa, umekumbwa na ucheleweshaji, na vikwazo tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka wa 2019 kutokana na matatizo ya kifedha, ambayo yameathiri utekelezaji wa mradi huo, na kunyima jamii ya eneo hilo uwanja unaohitajika; KWA HIVYO SASA, Bunge la Seneti, linaazimia kwamba Hazina ya Kitaifa na Wizara ya Maswala ya Vijana, Uchumi Ubinufu na Michezo, itengee Serikali ya Kaunti ya Mombasa, ruzuku ya masharti ya shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi uwanja wa Manisipaa wa Mombasa. Bw. Spika wa Muda, nimesimama kwa masikitiko kwamba ukanda mzima wa Pwani kwa sasa hauna uwanja wa kimataifa ambao unaweza kuchezewa mchezo wa mpira wa kimataifa. Uwanja ambao ulikuwa unatumika kwa muda mrefu ulikuwa ni uwanja wa Manisipaa ya Mombasa ambao ulijengwa kwa ufadhili wa Work for Aga Khan, mnamo mwaka wa 1957. Uwanja huu, uliandaa mchezo wa kimataifa mwaka wa 1962 wakati mchezo wa kwanza wa Gossage, ulichezwa. Gossage Cup ilikuwa inachezwa baina ya mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania. Baadaye iliitwa Confederation of East and Central African Federation (CECAFA). Mnamo mwaka wa 1962, Mombasa ilikuwa na uwanja wenye kiwango cha kimataifa, kwa wakati ule ambapo iliweza kuandaa michuano ya kimataifa. Vile vile,"
}