HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404958,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404958/?format=api",
"text_counter": 334,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "baada ya hapo, uwanja huu umeandaa michuano mingi ya kimataifa, hususan CECAFA ambapo timu za Kenya, Uganda, Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, zimewahi kucheza katika uwanja ule Na vile, mwaka wa 1996, uwanja huu uliandaa mechi ya kimataifa ya youth, ambao walikuwa washindi wa kwenda Olympic kati ya Kenya na Nigeria. Wachezaji wenye tajriba kubwa kama vile JJ Okocha na Nuan Kokanu waliweza kucheza katika uwanja ule. Ilizua hisia na uzalendo mkubwa kwa watu wa Kenya na watu wa Mombasa. Vile vile, uwanja huu umewalea wachezaji wengi kutoka Pwani. Vile, wengine walihamia bara, kwa mfano, marehemu, Ali Kajo, Marehemu, Ahmed Breik, Mahmoud Abass, ambaye alikuwa ni Kenya One kwa muda mrefu, na mwisho alichezea timu ya AFC Leopard, ambayo juzi, ililambishwa lolo na Gor Mahia hapa katika mchuano wa ‘Mashemeji Derby.’ Kwa hivyo, ni kiwanja kilicho na historia ya kusaidia pakubwa kuinua viwango vya mpira wa soka kabumbu katika eneo la Mombasa na Pwani kwa jumla. Ilipofika wakati wa ugatuzi, uwanja huu ulikuwa unasimamiwa na Baraza la Munispaa ya Mombasa. Ugatuzi ulipoingia, ukachukuliwa na Kaunti ya Mombasa. Nia na madhumuni ya Kaunti ya Mombasa ilikuwa ni kujenga uwanja wa kimataifa ambao utasaidia kuinua talanta katika eneo lile na kuandaa michuano ya kimataifa, ili kuleta biashara na maendeleo katika eneo la Pwani. Mnamo mwaka wa 2018, Kaunti ya Mombasa ilitoa mpango wa kuujenga upya uwanja ule na kutenga pesa za kutekeleza hilo. Mnamo mwaka wa 2017/2018, Kaunti ya Mombasa ilifanya vizuri sana katika ukusanyaji wa kodi Mjini Mombasa. Kwa lugha ya Kiingereza, inaitwa Source Revenue (OSR). Walifanya vyema mpaka Commission on Revenue Allocation (CRA) wakatoa ruzuku ya bilioni moja kama kiinua mgongo kwa Kaunti ya Mombasa kwa kukusanya pesa kupita matarajio yake. Kwa hivyo, mipango ilikuwa imefanya uwanja ule ujengwe kwa njia ya kudhibiti bajeti na kwa muda unaofaaa. Bahati mbaya ni kwamba Serikali Kuu ilipitsha amri mzigo mingi, ibebwe na Standard Gauge Railway (SGR). Kwa hivyo, biashara Mombasa ikaanguka na mapato ya Kaunti ya Mombasa pia yakaanguka. Baadaye, kukaingia janga la Korona mwaka wa 2020 mpaka 2021. Athari za Korona zikaathiri pakubwa, mapato ya Kaunti ya Mombasa na ya Serikali. Hivyo basi, ikawa Serikali ya Kaunti ya Mombasa haikuweza kupata pesa hizo. Hivi tunapo zungumza, imekuwa vigumu kwa Kaunti ya Mombasa kujenga uwanja huu kwa mkupuo mmoja. Zile pesa wanazoweka kwa bajeti yake, kwa mfano, bajeti ya mwaka jana, ilikuwa ni shilingi milioni themanini. Pesa hizi haziwezi kutosheleza ujenzi wa uwanja huu. Uwanja wenyewe umejengwa wa kisasa na utakuwa na uwanja wa mipira ya miguu, kidimbwi cha kuogelea cha hadhi ya Olympic, jumba la sanaa, ama auditorium ambalo litasaidia pakubwa kuinua sanaa, na pia jumba la mikutano., Uwanja huu utakuwa na uwezo wa kubeba, mashabiki, 18,000-20,000. Kwa hivyo, uwanja huu utakuwa wakimataifa. Kaunti ya Mombasa, ina hoteli na sehemu za kupumzika zenye viwango vya kimataifa. Kwa mfano, hoteli ya Serena, Whitesands,"
}