GET /api/v0.1/hansard/entries/1404960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404960,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404960/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Neptune na nyingine nyingi ambazo zina uwezo wa kubeba wageni wote watakaokuja kwa Kaunti ya Mombasa na kuhakikisha wamehudumiwa. Mwaka huu, Kenya itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mabunge ya East Africa. Mashindano haya yamepangwa kufanywa katika Kaunti ya Mombasa. Kwa hivyo, kiwanja hiki kitakuwa na umuhimu zaidi kikikamilishwa ili kitumike wakati wa mchezo hii ya Bunge za East Africa. Uwanja tayari umetengenezwa. Iliyobakia sasa ni kuleta vifaa uwajani. Kinachoweza kuchelewesha labda ni kutengeneza ule uwanja wenyewe utakaotumika kucheza kandanda. Kwa ujenzi wa mambo mengine, ni vitu vichache vya kuwekwa kwa pamoja. Ninamsihi contractor amalize uwanja huo ili uwekwe tayari kwa matumizi. Sehemu yote ya Pwani kama nilivyotangulia kusema, hatuna uwanja kama huu. Hivyo basi, uwanja huu hautasaidia Mombasa peke yake, lakini utasaidia Pwani nzima kwa jumla. Tumeona kwamba talanta zipo katika eneo la Pwani. Lakini, haziwezi kukua kwa sababu hatuna nafasi ya kuleta timu za kimataifa kuja pale kucheza. Hatuna nafasi ya kuwaalika wakufunzi na timu zingine kwa sababu hatuna viwanja vya kisawasawa ambavyo wakufunzi wale watasaidiana kuinua talanta katika maeneo yetu. Kutokana na ukosefu wa uwanja ule, hali ya kandanda imeshuka katika eneo la Pwani. Tumeona vijana wengi wameingilia mihadarati na itikadi kali. Mwaka jana, Kamati ya Seneti ya Uhasibu ilienda kutathmini. Ilizuru uwanja ule na kuona kwamba unahitaji kukamilishwa. Juzi Serikali Kuu ilimtuma Waziri wa Michezo, Sanaa na Masuala ya Vijana. Alipozuru uwanja huo, aliahidi kwamba atasaidia kuujenga. Kuna Hazina ya Michezo, yaani Sports Fund, ambayo inatumika hususan kusaidia kujenga miundombinu na kununua vifaa vya michezo katika nchi yetu. Tunaomba pesa kwa sababu tunajua kuwa Serikali ni jungu kuu na ina fedha ambazo inaweza kutusaidia kumaliza ujenzi wa uwanja huo kwa haraka ili uweze kutumika na wananchi waweze kufurahia. Kenya imepata fursa ya kuandaa michuano ya kombe la mabingwa barani Afrika mwaka 2027. Mombasa na sehemu zingine za Pwani ziliteuliwa kuandaa michuano hiyo muhimu. Mwaka 2004, tulikuwa mbele katika ujenzi wa viwanja za michuano hiyo. Ni makosa kunyimwa fursa kama hii kwa sababu hatuna uwanja wa kimataifa ambao unaweza kutumika. Suala la viwanja sio tu la watu wa Pwani pekee, bali ni suala la kitaifa kwa sababu Mombasa ni sehemu ya Jamhuri ya Kenya. Kwa hivyo, hatufai kuachwa nyuma. Serikali ya Jubilee iliyoondoka mamlakani ilikuwa imeahidi kujenga stadia nane; moja katika kila mkoa. Hakuna hata moja iliyokamilika. Wakati huo, Mhe. Rais wa sasa, alikuwa Naibu wa Raisi. Alizungumza hadharani kwamba watajenga stadium moja kubwa katika kila mkoa. Hilo halikufanyika. Sisi watu wa Mombasa tunaomba atupe ruzuku ya masharti ya bilioni moja nukta saba ili tuweze kukamilisha mradi huo muhimu ambao utasaidia pakubwa nchi ya Kenya."
}