GET /api/v0.1/hansard/entries/1404968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404968,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404968/?format=api",
"text_counter": 344,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Katika maeneo ya former Western Province kama vile Kakamega, viwanja vya mpira ni vingi kule. Hiyo ndio sababu vijana wengi kutoka Western Province ni wachezaji wa Harambee Stars. Jambo la kusikitisha ni kwamba kwa miaka mingi, timu za Kenya zimekuwa zikipata wachezaji na wakiambiaji wengi kutoka Pwani. Hata hivyo, tangu utawala wa Rais hayati Moi, sehemu hiyo haijakuwa ikizingatiwa. Kwa sababu hiyo, ukiangalia timu ya Harambee Stars, hakuna hata mtu mmoja kutoka upande ule. Ni jambo la kusikitisha kwamba sehemu iliyokuwa ikisifika sana zamani kwa kutoa wachezaji maarufu kama Ali Kajo, Sungura, Kadir Fara miongoni mwa wengine, imesahaulika. Walikuwa wachezaji katika timu ya Kenya. Kadir Farah alikuwa kiungo wa kati mzuri sana. Mwingine alikuwa Mahmoud Abbas. Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa sehemu hiyo imewachwa nyuma kimaendeleo. Namshukuru Sen. Faki kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ameona kwamba hakuna nafasi ya kuweka ndugu zetu katika timu ya Harambee Stars. Ingekuwa vyema Wizara ya Michezo, Sanaa na Masuala ya Vijana inayoshughulika na mambo ya michezo, hususan kandanda, kutanabahi kuwa uwanja ukijengwa, kutakuwa na watu wanaokimia, wale wa high jump na michezo mingine mingi inayofanyika ndani ya stadium . Mtu akiwa na talanta yoyote, anaweza kutumia nafasi hiyo kuendeleza talanta anayotaka. Natumai kutakuwa na wakati kama huo ambapo vijana watajihusisha na talanta kama ilivyokuwa zamani."
}