GET /api/v0.1/hansard/entries/1404973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404973,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404973/?format=api",
    "text_counter": 349,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Maanzo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13589,
        "legal_name": "Maanzo Daniel Kitonga",
        "slug": "maanzo-daniel-kitonga"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninaomba kuchangia Hoja hii muhimu. Mwaka wa 2008 hadi 2010 nilikuwa nimesimamia michezo hapa nchini. Kuna umuhimu kuwa na uwanja wa kimataifa kule Mombasa ambapo michezo inaweza kufanyika. Tulikuwa Rwanda kwenye michezo ya Bunge za Afrika Mashariki mwaka uliopita. Michezo hii ilipokuwa hapa nchini, ilichezewa Kaunti ya Mombasa na hakukuwa na viwanja vya kutosha kwa wachezaji wote. Mwaka huu Kenya itakuwa wenyeji wa michezo hii. Nahofia kuwa tutarudi Mombasa na hatuna viwanja. Ni muhimu kuwa na uwanja wa kimataifa mjini Mombasa. Hoja hii pia imeguzia swala la ruzuku ya masharti. Hizi ni fedha ambazo hupeanwa duniani ili kujenga viwanja vya kuchezea. Kuna aina nyingi ya michezo kama vile kandanda, netiboli na riadha. Ni muhimu sana kabla tupate wageni wa East Africa Community (EAC) Inter-"
}