GET /api/v0.1/hansard/entries/1404975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404975/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Maanzo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13589,
        "legal_name": "Maanzo Daniel Kitonga",
        "slug": "maanzo-daniel-kitonga"
    },
    "content": "tuwe na uwanja wetu kwani sisi sote tutaelekea Mombasa. Tutaenda Kaunti ya Mombasa ijapokuwa hakuna uwanja wa kimataifa, wala viwanja vya kutosha. Michezo kadhaa itachezewa kwa mashule. Jambo hili linafaa kuzingatiwa ili viwanja vilivyo kule Mombasa vipate wafadhili ili waweze kusaidia, tuwe na viwango vizuri vya viwanja. Kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale zinafaa zitenge fedha kwenye bajeti zao za kutengeneza viwanja vya kuchezea. Kuna talanta kubwa sana, hasa ya kandanda kule Mombasa. Nilipokuwa shule ya Upili ya Starehe, wachezaji bora zaidi wa mpira wa kandanda walitoka upande wa Pwani. Kulikuwa na mmoja aliyekuwa anaitwa Mohamed aliyekuwa mashuhuri sana kwa kandanda. Pwani, kuna talanta na inafaa zizingatiwe. Isikuwe tu wakati tunaomba kura; wakati wa siasa ndio tunaenda Pwani, Lakini wakati wa kugawa raslimali ya Kenya wakaaji wa Pwani wanakosa vitu muhimu kama uwanja wa mchezo. Inafaa tuwe na uwanja huu ili michezo mikubwa kama ambayo inatarajiwa ya kandanda 2027 mchuano mmoja ufanyike Mombasa. Wakenya wamezoea hali ya anga ya Mombasa ila wachezaji wageni wangepata ile joto wakicheza, kwani siyo nchi nyingi zina joto kama Mombasa. Pwani kuna bahari ambapo wageni wengi huzuru. Ili utalii uimarike nchini, ingekuwa vyema kwa watalii ambao wanapenda michezo wakizuru Pwani wanafanya mazoezi ya kukimbia, kandanda na mazoezi mengine kwenye uwanja huu."
}