GET /api/v0.1/hansard/entries/1404984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404984,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404984/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, sina uzoefu wa lugha ya Kiswahili lakini ninaunga mkono Hoja iliyoletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki. Viwanja vya michezo hapa nchini vipewe kipau mbele kwa ajili ya vijana. Ninaunga mkono sehemu moja ya Hoja alivyosema kuwa viwanja vitakavyotengenezwa katika sehemu mbalimbali za kaunti zetu zitasaidia vijana wapate mahali pa kufanya mazoezi ili wasitumie mihadarati na kufanya mambo ambayo siyo ya kistaarabu nchini. Kiongozi wa Walio Wachache katika Seneti ambaye ni hakimu mstaafu amesema kuwa Kaunti ya Nandi inajivunia kwa sababu ya kuwa na wanariadha waliobobea. Mwanariadha kama Kipchoge Keino na wale wengine wametoka Kaunti ya Nandi lakini hatuna viwanja vya michezo vya mazoezi. Ukiamka macheo utapata vijana wengine barabarani kule mashinani wakifanya mazoezi ya riadha. Jioni saa kumi na moja, ukiendesha gari ama kutembea kule mashambani utapata vijana wengine wanacheza voliboli. Hawana sehemu ama viwanja maalum ambavyo vimetengwa. Nashukuru Mhe. Rais William Ruto na Serikali yake kwa sababu mwaka jana, baada ya kuona kudhoofika na kuumia kwetu alitoa agizo kwa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo wajenge uwanja mpya mjini Kapsabet. Uwanja unaojengwa na serikali ya kaunti umejengwa zaidi ya miaka 14 kama vile jengo jipya la Bunge. Bajeti ya uwanja ule inaendelea kuongezeka. Ni aibu sana kuwa uwanja kwenye mji wa Kapsabet haujakamilika baada ya kutumia mabilioni ya pesa. Kwenye mji wa Nandi Hills, hakuna uwanja. Kukinyesha tu uwanja ulioko unaloa maji, vijana wanakosa nafasi ya kucheza. Uwanja huu unapaswa kujengwa na Serikali ya Kaunti ya Nandi lakini wamezembea. Kaunti ya Nandi imebarikiwa. Usiutazame mwili wangu huu, kwani nilikuwa mwanariadha shupavu. Karibu nishinde medali kwenye enzi zile zangu. Kaunti ya Nandi imebarikiwa na wanamichezo na wanariadha lakini hatuna uwanja uliotayari ili kuwapatia wanariadha na wanamichezo nafasi ya kufanya mazoezi. Gavana wa Kaunti ya Nandi alikuwa kwenye Kamati ya Seneti ya Uhasibu wa Fedha za Umma katika Kaunti."
}