GET /api/v0.1/hansard/entries/1404986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404986/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ni aibu sana kwa sababu kama Kaunti ya Nandi, tunajivunia kuwa na wanariadha na hatuna uwanja wa kimataifa. Kama ujuavyo, wanariadha waliobobea, Bw. Eliud Kipchoge na Bw. Kipchoge Keino wanatoka katika Kaunti ya Nandi. Bw. Henry Rono ambaye tulimuzika majuzi na tunaendelea kuiombea familia, pia anatoka katika Kaunti ya Nandi. Pamela Jelimo na Janet Jepkosgei ambaye watu wengi wamempa jina la utani, Eldoret Express, pia wanatoka katika Kaunti ya Nandi. Hata hivyo, ni aibu kwa Kaunti ya Nandi na serikali za ugatuzi kwa sababu zimezembea. Wameshindwa hata kujenga kiwanja cha mbuzi ambako wanaweza fanya mazoezi. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Nandi naona aibu kwamba tunaipigania hapa. Nimekumbushwa kwamba kamati yetu ya masuala ya fedha inaangalia bajeti na tunaendelea kupigania pesa."
}