GET /api/v0.1/hansard/entries/1404987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1404987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404987/?format=api",
"text_counter": 363,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, niko na sheria ambayo najaribu kuongeza asilimia ambayo inaenda katika kaunti, kutoka asilimia 15 mpaka 40. Ni aibu sana kuwa bilioni za pesa zimeenda katika Kaunti ya Nandi. Hata hivyo, Gavana wangu alipata muhula wa pili. Akiwa kule mashinani, alisema kwamba yeye hakushinda lakini alitumia mpira wa mkono ili apate muhula wa pili. Hiyo ndiyo sababu hatujaweza kuona maendeleo yeyote, hasa katika Kaunti ya Nandi. Nimeona Maseneta kama vile Sen. Abass na viongozi wa Walio Wengi na Walio Wachache Bungeni wakitaja Nandi. Kiongozi wa Walio Wachache amesema Nandi imejaa wanariadha. Lakini, hatuna viwanja vya michezo ambazo zinaweza tumika kuhakisha wanariadha wanafanya mazoezi ya kutosha. Ukienda katika Kaunti ya Uasin Gishu, utaona kiwanja cha 64 ambacho hakijakamilika. Ukienda katika Kaunti ya Elgeyo Markwet kuna uwanja wa mchezo unaoitwa Kamariny na kule Bomet kuna Bomet Green Stadium. Ninataka kumshukuru Mhe. Rais William Ruto na Serikali yake kwa sababu wakati tulisema Kericho Green Stadium ibadilishwe, imebadilishwa na kupewa jina la Kiburuku Chuma Wilson, ambaye alikuwa mwanariadha aliyebobea katika enzi zake. Ukienda katika Kaunti jirani ya Vihiga, Kisumu na sehemu za magharibi, tuko na wanariadha na wachezaji wa kandanda wengi walioheshimika. Kwa mfano, mchezaji maarufu Kadenge. Ndugu yangu Sen. (Dr.) Khalwale anatoka katika eneo la magharibu. Ni afadhali Kakamega wako na uwanja ambao wanaweza kutumia kufanya mazoezi. Hata hivyo, ulitengenezwa na Gavana aliyetoka. Kama Bunge la Seneti ni lazima tuchukuwe msimamo kidete na kuhakikisha kaunti zetu zimeweze kujua kwamba masuala ya michezo yamegatuliwa. Wachukuwe hatua kabambe na wahakikishe kwamba zile pesa ambazo wanaweka zinatumika kukuza talanta pale mashinani. Talanta Hela ilikuja na tunataka tujue inatumika vipi ili kuhakikisha vile viwanja ambavyo vinatakikana kujengwa katika taifa letu la Kenya vimejengwa. Tunapojitayarisha kwa dimba linalo kuja, najua Kaunti ya Mombasa, kaunti za kule magharibi kama vile Kakamega, Eldoret na nchi ya Uganda na Tanzania wanaweza"
}