GET /api/v0.1/hansard/entries/1404989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1404989,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404989/?format=api",
    "text_counter": 365,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "kupewa nafasi ya kushiriki katika hilo dimba la mpira ambalo. Ni lazima tuwe tayari ikiwa dimba hilo litafulu. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi Naibu wa Rais, Mhe. Rigathi Gachagua anapambana na mambo ya madawa ya kulevya na miharadati katika taifa letu la Kenya. Tukitaka kuangamiza janga hilo ni lazima tuhakikishe viwanja na kumbi za michezo zimetengenezwa ili vijana wapate mahali pakupata uraibu wa michezo mbalimbali katika taifa letu la Kenya. Nilikuwa na hoja tatu. Tunapoelekea katika michezo ya Olimpiki mwaka huu kule Paris, Ufaransa, nataka kuwaomba Wakenya tupeane ufadhili ambao tukonao ili kuhakikisha wanariadha ambao wanaelekea huko wamepata ufadhili wa kutosha ndio waweze kutuletea medali. Wakati wa wikendi, mwana riadha aliyebobea, Peris Chepchirchir, aliweza kuvunja rekodi mpya kule London. Hii ndio maana ninataka tuwape changamoto kwa kuwapa viwanja nafasi ya kutosha kufanya mazozi katika viwanja vyetu. Wakati tunaelekea muda wa michezo wa mwaka huu, wanariadha hawastahili kuwa na shida zozote. Tuliona yule murusha mkuki, Bw. Yego, alikuwa ameanza kuombaomba katika mitandao ya kijamii. Hiyo ni aibu sana ikizingatiwa tuko na kikapu maalumu ya mambo ya michezo katika taifa letu la Kenya. Nataka kumwambia Waziri wa Michezo kuwa tunamtegemea kuhakisha zile pesa za kusaidia hawa wanamichezo zinatumika vilivyo. Jambo lingine ni kuhakikisha tumefanya uchaguzi ya wale wanaosimamia riadha, voliboli na michezo mingine. Nimefurahi kuwa wakati kuliwa na mchezo wa ‘mashemeji’, ndugu yetu kinara wa Azimio alienda kuangalia mchezo huo ingawa hakuenda mazishini. Hata hivyo, tulikuwa tumeambiwa na ndugu yake kuwa alikuwa hajisikii vizuri. Nimefurahi kwa sababu walikusanya zaidi ya shilingi milioni nne nukta tano. Ikiwa tunataka tuweke viwanja vya mchezo, pesa zinazochukuliwa zinaweza kutosha. Bw. Spika wa Muda, naunga mkiono Hoja hii. Ninataka niwahakikishie wananchi wa Kenya na wanariadha kwa jumla, kuwa kama Bunge la Seneti tutafanya kazi pamoja. Nikimalizia kwa zile dakika chache ambazo zimebaki, nimemuona Seneta wa Narok. Jana nimeona katika mitandao kwamba kuna wale waakilishi wadi ambao wanapigwa katika mahafla pale mashinani wakati wanajaribu kuuliza maswali. Niliona mwakilishi wadi wa Mara ambaye anaitwa Kipng’eno Simba, akizabwa makofi. Hii si mara ya kwanza. Nilikuwa ninaona Gavana Tunai aliyetoka alikuwa na heshima kwa maswali. Gavana ole Ntutu ameanza kuwa mtukutu na hauwezi kumuuliza swali. Kwani Kaunti ya Narok iko Kenya ama inaendeshwa na wabeberu au wafedhuli? Lazima nimuulize Seneta wa Kaunti ya Narok alete Hoja hapa Seneti, kwa sababu hiyo ndiyo inaweza kuwa njia moja ya mtu kubanduliwa ofisini."
}