GET /api/v0.1/hansard/entries/1405001/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1405001,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405001/?format=api",
    "text_counter": 377,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Olekina",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 407,
        "legal_name": "Ledama Olekina",
        "slug": "ledama-olekina"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii itakayotuwezesha kuzingatia umuhimu wa talanta ya vijana wetu, ambao wengi wao katika Kaunti ya Mombasa, hujipata wameenda baharini. Kama kungekuwa na Stadium ambayo wangeenda kukimbia, pengine tungepata wakimbiaji wengine kutoka Mombasa. Wakati Mhe. Faki aliponiuliza nichangie Hoja hii, kuna jambo fulani nililolifikiria. Ni kweli kabisa kwamba tuna kaunti 47 na tuko na talanta nyingi katika Kenya hii. Je, wakati mwengine inatubidi tuangalie kaunti zote za Kenya tuone ni gani haina hivi viwanja vya michezo? Bw, Spika wa Muda, utaniwia radhi kwa sababu Kiswahili ni lugha geni kwangu, lakini nitajaribu tu."
}