GET /api/v0.1/hansard/entries/1405007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1405007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405007/?format=api",
    "text_counter": 383,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Olekina",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 407,
        "legal_name": "Ledama Olekina",
        "slug": "ledama-olekina"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, tulikubaliana na Kiongozi wa Walio Wachache kwamba, nikiwa nazungumza hapa ananisikiliza ili nikipotea ananisaidia. Lakini sasa ameanza kuzungumza na Sen. Wambua. Hii ni shida kubwa sana. Naunga mkono Hoja hii ya kuweka fedha za kujenga stadia . Lakini jambo ambalo lazima tulitilie maanani ni, je, wakati tumetenga fedha kadhaa, jukumu la kaunti litakuwa lipi, ili kuhakikisha hizi stadia hazitakuwa zile watu wanasema, “ white elephantproject?”. Ni lazima tutenga fedha za kujenga kiwanja, isikuwe “ndovu mweupe” ama ile nyumba kubwa ambayo imejengwa tu. Naunga mkono tutafute pesa za kujenga stadia, lakini tukiweka hizo pesa, ni lazima kila mwaka tuchangie pesa zingine za kuhifadhi zile stadia . Hii ni kwa sababu tunaweza kufurahi na kuchanga pesa na tuweke hata bilioni mbili. Lakini, tukishafanya hivyo, sisi kama Wakenya tunajua ile shida hutokea. Mara contactor hajamaliza hiyo"
}