GET /api/v0.1/hansard/entries/1405018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1405018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405018/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, mngenikubalia niongee Kiingereza kwa hii Hoja, ningechangia mpaka mjue ukweli ya kwamba ni lazima tufanye kazi tukiketi hapa. Tujiulize kama kiwanja kinachojengwa kitadumu na kama zile pesa tunazotenga zimefanyiwa utafiti ili kujuwa kama zinatosha kwa uchumi wa sasa. Gunia la simiti sasa ni shilingi mia tisa. Mbali na zile pesa tunazotenga ili tujenge viwanja, ni vizuri pia tutenge kiwango fulani ili tuhifadhi viwanja vile. Nakumbuka wakati ambao County Governments zipobuniwa, kuna kaunti ambazo hazikuwa na makao makuu, ambazo Seneti hii ilitenga pesa ndio zijengwe. Ukiangalia hizo zote, ni chache sana zilizomalizwa. Kuna zengine ambazo bado hizo projects hazijawahi kukamilika. Ni lazima tutilie hayo maanani. Bw. Spika wa Muda, Kiswahili ni kigumu. Wacha nimalizie hapo. Mungu awabariki."
}