GET /api/v0.1/hansard/entries/1405021/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1405021,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405021/?format=api",
    "text_counter": 397,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Khalwale",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 170,
        "legal_name": "Bonny Khalwale",
        "slug": "bonny-khalwale"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Naomba kuchangia Hoja hii. Kabla sijatoa maoni yangu, namshukuru ndugu yangu, Sen. Faki na aliyemuunga mkono, Sen. Madzayo. Haya maneno ya Mombasa Stadium sio ya kufanyia mchezo. Ujenzi wa uwanja huo ulianza kabla tupate Uhuru katika nchi yetu ya Kenya. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa successive governments zimekataa kufadhili ili kuboresha uwanja huu wa kitaifa. Bw. Spika wa Muda, siwezi kulaumu Serikali ya Kitaifa pekee. Serikali ya Kaunti ya Mombasa pia imechangia haya. Ndugu zangu wengine hawakuwa hapa. Mimi nilikuwa katika hii Seneti nilipomuona aliyekuwa Gavana, Mhe. Joho, akichukua hundi la milioni mia tano ya kujenga hiyo stadium. Bejeti hiyo ilipitishwa. Leo hii, watu wa pwani, hasa kutoka Mombasa, ambao wananisikiza wanafaa kumuuliza Mhe. Joho kule pesa hizo zilienda. Tunaweza kutaka"
}