GET /api/v0.1/hansard/entries/1405038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1405038,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405038/?format=api",
"text_counter": 414,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Spika wa Muda, Kanuni za Kudumu za Seneti zinasema kuwa huwezi kumtaja mtu ambaye hayuko ndani ya Bunge hili kwa sababu hawezi kujitetea. Vile vile, hufai kumtaja mtu ambaye hakupewa taarifa kuwa anahitajika kujitetea. Seneta alisema kwamba Bw. Joho alionekana akibeba kitita na kuwa pesa zile hazikutumika vizuri. Je, ni sawa Seneta ambaye ninaenzi sana, ambaye pia ni Kiranja wa Walio Wengi, kusema kuwa aliona Bw. Hassan Joho akiwa amebeba kitita, ilhali hayuko hapa wala hakuulizwa aje hapa ili ajitetee?"
}