GET /api/v0.1/hansard/entries/1405054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1405054,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405054/?format=api",
"text_counter": 430,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kumweleza ndugu yangu kiongozi ambaye anapambana na “Bullfighter” kuwa kama Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Pesa za Umma, niliongoza jeshi la Maseneta kuzuru Kaunti ya Mombasa. Tulipofika huko, tulipata kuwa ule uwanja wa michezo ulikuwa umebadilika na kuwa mahali pa wanyama kuishi. Kuna “majisimba” na “majizimu” katika uwanja huo ilihali, katika bajeti na hesabu za ukaguzi, kuna zile stakabadhi zote za kuonyesha kwamba, wakati Mhe. Joho alikuwa Gavana katika kaunti ya Mombasa, aliweka zaidi ya shilingi milioni mia tano."
}