GET /api/v0.1/hansard/entries/1405089/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1405089,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1405089/?format=api",
"text_counter": 465,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kwanza kabisa nimpongeza Seneta wa Machakos, Sen. Kavindu Muthama, kwa Hoja hii. Niseme ni kweli kabisa, barabara, daraja, mimea na vikingi vya simu zimebebwa na maji. Kila mahali, haya mafuriko yameleta mahangaiko. Kile ambacho ni cha kuvunja moyo sana ni kwamba kulikuwa na tetesi ya kwamba kaunti zetu zimejikimu vilivyo baada ya kuambiwa na watabiri wa hali ya anga ya kwamba kutakuwa na haya mafuriko. Walisema wamejiandaa vilivyo. Lakini kile tumeona ni watu wetu wakiumia. Shule na barabara zetu zinabebwa na maji. Kisa na maana, hakuna jambo lolote linaonyesha watu walikuwa wamejitayarisha. Mitaro imejaa maji na ilhali tulikuwa tumeambiwa na gatuzi zetu ya kwamba wamejiandaa. Mitaro imetengenzwa na hakutakuwa na shida kama hii. Swali ninalo jiuliza na linanisumbua sana ni katika vyuo vikuu vyetu tunafundisha wahandisi. Sijui ni kazi gani wanafanya kwa sababu hata mahali ambapo huwezi ukapata maji yamejaa, barabara zetu tayari zinabebwa na maji. Sio hilo tu. Ningependa Serikali kuu ichukue jukumu na kufanya jambo hili liwe la dharura. Baada ya haya mafuriko, kutakuwa na shida nyingi kama ukosefu wa chakula kwa sababu mimea yetu tayari imebebwa na maji. Utapata shida katika shule zetu. Magonjwa yataanza. Utasikia kuna ugonjwa wa Cholera na magonjwa mengi ambayo yataletwa na hali ya kutokuwa na usafi kwa sababu ya maji ya gharika. Jambo la kuvunja moyo sana ni kuwa kila wakati kuna haya mafuriko, ni jambo linalojirudia. Inaonyesha kwamba sisi katika Seneti kazi yetu ni kugawa pesa ilhali hazitumiki jinsi zinapaswa kutumika na gatuzi zetu. Itakuwa ni mazoea. Baada ya mafuriko kuisha, hakuna jambo lingine litakaloendea. Shughuli itakuwa ni kutafuta pesa za dharura ili kuleta uadilifu kwenye barabara za magatuzi yetu. Sio hilo tu bali pia hata shule zetu za chekechea na barabara ambazo sisi tunazishughulikia katika Seneti. Hii iwe funzo. Kama alivyosema Sen. Wambua, hata Barabara ya Expressway ilikuwa imejaa maji. Hilo halikufanyika katika nchi ya Kenya pekee. Ilifanyika pia kule Dubai. Uwanja wa ndege ulikuwa umejaa maji. Nilidhani kuwa kule wameendelea lakini nikakumbuka kuwa pahali pasipopangwa panaweza kujaa maji. Leo asubuhi niliambiwa na ndugu yangu kwamba kuna vitu viwili ambavyo havisahau. Ndovu anapopita mahali, huwa hasahau. Maji vile vile hayasahau mkondo wake. Jambo hili linanifurahisha. Sen. Methu na kamati yake huwa wanashughulika sana na watu wanaouza mashamba. Huu ndio wakati mzuri mtu kuangalia mahali alipouziwa. Katika lugha ya kina Sen. Methu, wanasema magutamaguta . Sijui iwapo hivyo ni kusema mafutamafuta. Unapoangalia mahali ploti kama hizo ziko, utaona vikingu tu kwa sababu ploti ambazo wananchi wa Kenya wamekuwa wakiuziwa zimejaa maji. Ni wakati ambapo sisi kama Seneti tunapaswa kuleta mabadiliko na kuangalia vizuri---"
}