GET /api/v0.1/hansard/entries/1406044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406044/?format=api",
    "text_counter": 372,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi niongee kidogo kuhusu Mswada huu ulioko mbele yetu. Mwaka wa 1963, Kenya ilipopata Uhuru, kulichaguliwa Maseneta 41. Maseneta hawa walikuwa wanasimamia majimbo yao. Katiba ya kwanza ilikuwa imepeana nguvu kwa majimbo. Siasa hii ya majimbo iliendelezwa na wakubwa wetu waliotutangulia kama Ronald Gideon Ngala, Masinde Muliro na Daniel Moi waliokuwa kwa Chama cha Kenya African Democratic Union (KADU). Hayati Mzee Jomo Kenyatta na Jaramogi Oginga Odinga walikuwa kwa Chama cha Kenya African National Union (KANU). Walitaka Serikali moja. Hawakutaka hata Seneti iwepo. Mpango uliotumika hasa ni kuyanyima majimbo pesa ili yafe kifo cha kawaida. Walitumia pia njama ya kuvunja KADU nguvu kwa kuwaringisha mikono wale viongozi ili Maseneta wahame. Walihama na kuingia upande wa Serikali na hatimaye wakateuliwa kama Wabunge wa kawaida. Kuua gatuzi zetu ambazo tuko nazo wakati huu, njia inayotumika ni kuzinyima pesa. Sisi hapa kamati yetu imekaa na kuangalia sababu nyingi. Mwenyekiti wetu Ali Roba amezielezea kwa undani, singetaka kurudia tena. Kisha akasema kwamba sisi kama kamati ya Seneti, tumekaa na kusema pesa ambazo zingefaa ziende kwa gatuzi zetu ni shiling billioni mia nne kumi na tano nukta tisa. Hawa wengine wameleta Mswada huu na kusema pesa zinayofaa ziende haswa kutumia maelezo ya Hazina ya Kitaifa ni shilingi bilioni mia tatu tisaini na moja. Nakubaliana kabisa na wenzangu ambao wamesema hapo awali ya kwamba wakati huu ni lazima tusimame kidete. Sisi sote tuseme ripoti hii ya Kamati yetu ya Fedha na Bajeti, tunaiunga mkono. Tusiangalie tuko mrengo gani wa kisiasa katika Seneti. Na sababu ni kwamba, ukiangalia sheria hii, Kipengele cha tisa kinaelezea sababu tisa ambazo Hazina ya Kitaifa wametoa tupeleke kwa gatuzi ni shilingi bilioni mia tatu tisaini na moja (Kshs391 bilioni). Lakini moja ya hizo sababu ukiangalia Kipengele cha 9(b) (c) wamesema umaarufu wa sarafu ya Kenya inashuka kwa sababu ya hali ya biashara ulimwenguni. Ninaomba wenzangu msome, Kipengele cha 9(e). Wanasema sarafu ya Kenya inashuka eti kwa sababu kuna vita Ukraine na Urusi. Imeandikwa kwa Mswada huu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}