GET /api/v0.1/hansard/entries/1406045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1406045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406045/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tunaouzungumzia leo. Kama waliziandika sababu hizo kwa sheria na kusema hizo ni kati ya sababu ambazo wanazitumia kugandamiza gatuzi. Hivyo basi, mgao unaofaa ni Shilingi 391 bilioni. Tunataka kuambia Hazina ya Kitaifa kwamba sababu hizo hazina maana tena wakati huu. Sarafu ya Kenya imepata nguvu na sababu walizotoa zimepitwa na wakati. Ni kweli sheria tunayoizungumzia sasa hivi na wakati walipopendekeza kiwango cha mgao huu, sarafu ya Kenya kweli ilikuwa hafifu. Lakini, sasa hivi, sarafu ya Kenya imeimarika. Kwa hivyo, zile sababu za kimsingi ambazo Hazina ya Kitaifa ilitumia ili kugandamiza mgao wa pesa za kutosha, mbali na yale makosa walifanya wakati wanafanya mahesabu ya base, walisema ya kwamba sarafu ya Kenya imezorota. Lakini sasa hayo mawazo hayapo tena. Kwa hivyo, tunawaomba wale wanaosema kupitia sheria hii ya kwamba pesa iwe ni Shilingi 391 bilioni, hatutaki hivyo. Wakubaliane na hali iliopo saa hii. Kamati ya Seneti imesema hali iliopo sasa, mgao wa gatuzi zetu 47 ni Shilingi 415.9 bilioni. Mimi nataka kusema jambo moja. Ni kweli kuna shida katika kaunti zetu. Kwa mfano, Tana River na nyinginezo ziko na shida. Lakini hata kama tuko na shida kwa boma zetu kuhusu matumizi ya pesa, hiyo sio kusema baba ambaye anaenda kuchukua mshahara, basi mshahara wake upunguzwe. Ule mshahara lazima uje wote jinsi inavyotakikana. Zile shida za kule nyumbani, tutazifuatilia na kuzitatua. Kama baba wa nyumba ni mlevi na anapeleka pesa kwa watu wasiohusika na hiyo familia, anaharibu pesa za familia, hayo ni mambo ya kule nyumbani. Tutayatatua. Tutamuitia wazee na tutamfunga. Lazima tumrekebishe. Hata hivyo, hatuwezi kwenda kwa ofisi yake tuseme mshahara wake upunguzwe. Kuna mazungumzo ambayo watu wengine wanasema serikali za kaunti zinatumia pesa zao vibaya. Hivyo basi, tupunguze ili haki inayotakikana ifanyike kwao. Mimi nasema hizo shida tutaziangalia kama Seneti na tutajaribu kuzitatua. Lakini, ule mgao wetu wa sawa kwa kaunti zetu hatutaki ukatwe. Tunawaomba wale walioleta Mswada huu wakitumia mwongozo wa Hazina ya Kitaifa waambie Hazina ya Kitaifa ilikosea. Yale mapendekezo na maelezo waliweka katika sheria hii imepitwa na wakati. Wakati huu, sarafu ya Kenya imeimarika. Tunataka sasa yale mapendekezo ambayo yametoka kwa kamati yetu yafanyike. Sisi kama Seneti, tushikane na tusimame pamoja na tuseme pesa zetu za kaunti ni Shilingi 415.9 bilioni. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}