GET /api/v0.1/hansard/entries/1406227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1406227,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406227/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Jambo la pili, Mswada huu pia unazungumzia mchakato wa mapito wa mipaka ya uchaguzi. Tunajua kila baada ya muda fulani lazima kuwe na mchakato wa mapito ya uchaguzi ili tuangalie mipaka ya uchaguzi ili kuhakikisha usawa na kuzuia udanganyifu. Vile vile tunapozingatia suala kama hilo, tutahakikisha kwamba ile mipaka itakavyoamuliwa ndio itakayowekwa rasmi kwa mambo ya uchaguzi, ndiposa tuzuie mambo ya udanganyifu. Ibara 89 ya ripoti ya NADCO inazungumzia kufanya marekebisho ili kuhakikisha Bunge linaongeza muda ili Bunge lipate nafasi mwafaka ya kuzingatia mambo haya ya mipaka ya uchaguzi. Pia Mswada huu unazungumzia mchakato wa kufanya maamuzi kwa sababu kulikuwa na tetesi nyingi sana katika uchaguzi uliopita. Watu walikuwa wanashangaa kama uamuzi utafanywa na watu wachache au watu wengi au kwa kauli moja. Maamuzi sasa itakuwa ni kauli moja. Wakati wanataka kufanya maamuzi katika tume la uchaguzi, lazima iwe ni kwa kauli moja, ile kwa Kiingereza tunasema unanimously ama iwe kwa wingi wa wanatume. Waswahili wanasema ‘wengi wape’. Wale ambao watakuwa wengi kwa maamuzi ndiye watafanya maamuzi katika tume ya uchaguzi."
}