GET /api/v0.1/hansard/entries/1406230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406230,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406230/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Vile vile Mswada huu unazungumzia mageuzi ya uchaguzi. Kutakuwa na ukaguzi wa orodha ya wapiga kura na utazuia wafanyikazi wa tume ya uchaguzi kufanya uchaguzi katika vituo ambavyo havijawekwa kirasmi, ama kwa Kiingereza havijakuwa gazetted . Hapo nyuma kumekuwa na utesi Mwingi sana, hata ikaleta michafuko na sintofahamu ya kwamba pengine kuna sehemu ambazo hazikuwa zimewekwa rasmi na watu wakapiga kura pale na hesabu ikajumulishwa kinyume cha sheria. Mswada huu unazungumzia zile taratibu ambazo zitafuatwa kukagua orodha ya wapiga kura kinagaubaga na kuhakikisha kuwa vituo vya kupiga kura ni vile ambavyo vimewekwa kirasmi kupitia sheria na vinatambulika na wapiga kura na wale wanaopigiwa kura. Hiyo pia italeta uwajibikaji. Kuna marekebisho yale tuliyazungumzia mwaka wa 2023 ya kwamba kuna wakati mwingine wafanyikazi wa tume walikuwa wanakawia kutoa uamuzi kuhusu washindi ama kunakuwa na sintofahamu kuhusu idadi ya kura wanayopata. Mswada huu unazungumzia zile taratibu na vile vitakavyofuatiliwa na kwa wakati gani uamuzi lazima ufanywe, ama ile tunaita declaration of winners kwa lugha ya Kiingereza. Saa zingine nafafanua kwa lugha ya Kiingereza kidogo ili wenzangu waelewe vizuri. Nazungumzia hili kwa sababu kumekuwa na tetesi na malalamiko. Watu wengine wameenda kortini na kulalamika kwamba uchaguzi haukufanyika kwa taratibu ambazo zinatakikana. Imefikia watu kupigana katika vituo vya kupiga kura, haswa zile sehemu za kutangaza maamuzi yale ya mwisho ya wale ambao wameshinda. Katika kuleta mawiano katika taifa letu la Kenya baada ya uchaguzi na baada ya kuwa na michafuko mingi sana… Majina ya watu wengi yameharibika, kama Chebukati ambaye amelaumiwa kwa mambo mengi. Mengine ni ya kweli. Mengine labda ni ya kuongezwa. Lakini kulikuwa na sintofahamu kubwa sana mpaka ukaleta maandamano na mambo mengi sana katika taifa letu la Kenya. Hivyo basi ni wakati mwafaka wa kupiga msasa taratibu hizo kupitia Mswada huu ili tuone ya kwamba jopo hili la kuunda Tume la Uchaguzi litatengenezwa kwa njia ya uwiano. Wale ambao wanasimama kwa vyama vya kisiasa na wale ambao watasimama kwa wao binafsi bila kutegemea chama chochote watapata usawa na afueni katika mambo ya uchaguzi. Mambo ya uchaguzi yanaweza kutuweka sawa na amani au kutugawanya kwa misingi ya kisiasa au misingi ya vyama vya kisiasa au misingi ya kijamii na kuleta athari kubwa kwa amani katika taifa letu la Kenya. Nawapongeza wale wote waliochaguliwa katika jopo la NADCO ambao wameshirikiana sana na kuzungumzia kwa kinagaubaga suala hili la Tume ya Uchaguzi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}