GET /api/v0.1/hansard/entries/1406231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406231/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Tukifanya uchaguzi mwaka wa 2027, zile changamoto tulizozipata zitakuwa hafifu. Pia mtu atajua kweli taratibu zimefuatwa kwa njia ya usawa. Wakati ule tulikuwa na shaka ikiwa makamishena watatu wanasema maamuzi ni haya na wengine wanne wanasema maamuzi ni yale. Sasa, je, tutafuata maamuzi ya watatu au wanne au tutafuata njia gani? Mswada unasema kwa hakika kwamba maamuzi yatakuwa kwa kauli moja ya wote kama makamishna wa Tume ya Uchaguzi ama itakuwa kauli ya wale walio wengi? Sisi kama Wakenya tutafuata uamuzi huo. Vile vile kuongeza jopo liwe na watu tisa inamaanisha tutapata taaluma zingine. Uchaguzi hauhitaji mtu wa tajriba ya uchaguzi peke yake. Kuna mambo mengi sana. Lazima tuwe na watu ambao wana tajriba nyingine ya kuongoza ile tume. Tume ya Uchaguzi ina changamoto nyingi sana. Lazima tupate wale ambao wana tajriba ya hali ya juu ya uongozi na wakati kuna shida wanaweza kuleta amani ndani ya ile Tume ya Uchaguzi. Naunga mkono na kuwashukuru sana wanakamati wa NADCO. Najua tulipanga jambo hili sisi wenyewe kama Wabunge na tukakubaliana ya kwamba twende njia hii. Lakini, tunaona kuna sintofahamu na wengine wanasema hivi na vile. Katika taifa la Kenya, tunataka kusonga mbele. Tukisema marekebisho ni haya na taratibu ni hizi, basi sote kwa kauli moja tuweze kushirikiana. Ili wakati wa uchaguzi aliyechaguliwa kama mshindi na aliyeshindwa, wapeane mikono kwa amani na wakubali kuongoza taifa letu. Tusiwe na misukosuko, sintofahamu, vita, mauaji na kupoteza vijana. Wakati huo tulipoteza Wakenya wengi sana. Haswa, vijana ambao tunawatarajia katika maisha ya sasa na baadaye. Hatutaki kurudi tulikokuwa tena. Kwa hivyo, lazima jopo hili lifuate taratibu ambazo zimewekwa na NADCO ambazo sisi wenyewe tumepitisha. Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu."
}