GET /api/v0.1/hansard/entries/1406277/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1406277,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406277/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria East, UDA",
"speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Matukio ambayo yamekumba nchi hii siku za hivi karibuni yameleta Mswada ambao uko mbele ya Bunge hili wakati huu. Lakini matukio hayo yamefuatia matukio mengi ambayo yamekuwa tangu nchi hii ilipopata uhuru. Kila uchaguzi ukimalizika, kunakuwa na nafasi ya Wakenya kuangalia, kuchambua na kurekebisha, kuzidisha, kuboresha na kuendeleza jinsi uchaguzi unafanywa katika nchi hii. Hivi karibuni, tulikuwa na uchaguzi ambao ulikuwa na tetesi nyingi sana zilizoleta mchakato huu ambao leo tunauzungumzia. Hatukubaliani na kila kitu ambacho kilitokana na mchakato wa NADCO lakini kwa sababu ni lazima Kenya iendelee kusonga mbele, baadhi ya mambo ambayo yametokana na hiyo ripoti inatubidi tuyazungumzie na kukubaliana nayo."
}