GET /api/v0.1/hansard/entries/1406278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406278,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406278/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
    "speaker": null,
    "content": "Ili kuendeleza mchakato kuhusu jinsi uchaguzi utaendelea kufanywa katika nchi hii, inabidi tukubaliane na mambo machache ingawaje kuna nafasi ya kurekebisha baadhi ya mengineo. Ikumbukwe ya kwamba sio zamani, nafikiri ni mwaka wa 2016, kulikuwa na uchaguzi Marekani. Wengi wetu tunaona Marekani kama nchi iliyokomaa kidemokrasia. Demokrasia yao imekomaa kwa takriban miaka 200 kufikia sasa lakini, pamoja na hiyo, kulikuwepo na matukio sawia na yale yaliyotokea nchini Kenya tulipofanya uchaguzi mwaka wa 2022. Hiyo ni kumaanisha kwamba bado mapendekezo yako hata tukirekebisha jinsi gani kulingana na Ripoti iliyotolewa na Kamati hii ama hata na National Dialogue Committee yenyewe. Tatizo sio sheria. Tatizo ni ubinafsi na fikira za watu. Hakuna demokrasia inayoweza kusazwa kwa hili jambo kama demokrasia ya Marekani, ambayo ina miaka mingi. Hili jambo linaweza kuibua matatizo kama yanayoendelea hadi katika mahakama."
}