GET /api/v0.1/hansard/entries/1406280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406280,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406280/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
    "speaker": null,
    "content": "tuheshimu kwamba amefuata sheria zilizowekwa akitoa uamuzi. Utakuwa uamuzi wa kubainika. Hilo ni tofauti na kuweka mikangamo na mifumo kama hii ya kielektroniki na mingine ya kuendesha chaguzi. Bila sisi kuwa na imani na yule aliyewekwa pale kufanya uamuzi ule, itakuwa bado ni bure. Tutatumia hela nyingi kutengeneza systems nyingi za kielecrtoniki na nyinginezo. Itakuwa bure bila sisi kumkubali huyu bwana na kukubali kwamba maamuzi anayotoa ni sahihi kisheria, yametosha na ni ya mwafaka. Tunaheshimu mahakama zetu. Naunga mkono Mswada huu lakini Bunge hili lisipoweza kufanya kazi yake vilivyo, tutakuwa tumetoa nafasi kwa mahakama kutunga sheria kwa niaba yetu. Niruhusu niseme kwamba ukabila ndilo tatizo letu nchini. Ni matatizo ya walio wengi na walio wachache. Ni shutuma na namna ya kuangalia yanayokupendeza. Unayavuta upande wako. Hujali masilahi yanayosaidia wingi wa watu. Hayo ndiyo matatizo. Kwa bahati mbaya, hatuyazungumzii. Walio na sauti kubwa wanapata nafasi yao kwa sababu wanaweza kwenda barabarani na kufanya fujo. Hatimaye, wao husukuma mambo yao yakafika katika upeo wa kitaifa. Wao husukuma sauti yao ikasikika na watu wote wakafuata hayo wakifikiri ndivyo inafaa kuwa. Kwa hivyo, ninakubali na kuunga mkono Mswada ili tuendeleze demokrasia. Tunaendelea kwa kila hatua. Tunaweka tofali baada ya jingine tukienda mbele. Mwisho ni kuhusu maeneo bunge. Tumefika sehemu ambayo tutasema tuko kwa hatari na kwamba tumekiuka sheria na Katiba. Bila kuwepo sheria ya kupanua yale maeneo bunge mia mbili tisaini na kutatua jambo hili la Tume ya Uchaguzi na Mipaka kwa haraka, tutakuwa pia tumepitwa na wakati hata tukifanya ule mchakato wa kuyaangalia upya. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu wa marekebisho ambao nimeusoma. Haifai kwamba muhula wa yule mwenyekiti uwe miaka mitatu. Inabidi tumpe muda mrefu zaidi. Isiwe muda wake unaisha wakati chaguzi zinafanyika. Tuweke muda ambao hautakwisha katikati ya chaguzi na awepo ofisini wakati tunatathmini historia ya chaguzi ambazo zimepita. Yaani, huyu bwana awe ofisini wakati tunachambua chaguzi na utendakazi wake. Ikiwezekana, aongezwe muda. Iwapo haongezwi muda, aondolewe . Vile vile, namna ya kumwondoa isiwe ya kuletea nchi utata. Nawachia hapo nikisema asante kwa kunipa nafasi. Vile vile, naunga mkono kuwe na nafasi ya marekebisho ya kuboresha zaidi tunapoendelea mbele. Asanteni sana kwa kunisikiza."
}