GET /api/v0.1/hansard/entries/1406366/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1406366,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1406366/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia Mswada huu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka. Kwanza Nachukua fursa hii niunge mkono na nipongeze Kamati iliyohusika kwa kuja na marekebishi ya sheria hii. Kwa hakika, ningeanza kwa kuunga mkono muda wa miaka mitatu kwa Mwenyekiti na wanakamati wengine ama Makamishna wengine. Huu ni muda wa kutosha na kama amefanya kazi nzuri, hakuna sababu ya kutoongezewa muda wa kuendelea. Hivyo basi sio lazima iwe miaka sita au tisa, kunao wengine na kila uchao, tunasema vijana ni viongozi wa kesho. Hiyo kesho itafika lini ikiwa tutashikilia tu kuwa wazee washikilie nyadhifa ambazo pengine wakati wao wa kupumzika umefika ili vijana wachukue hatamu hizo? Naunga mkono kiwango cha wale ambao wanaweza kupitisha jambo. Idadi yake ni watano. Hii itatupatia nafasi mwafaka itakayokuwa inaonyesha dhahiri kwamba yale ambayo wamepitishwa ni yale ambayo wananchi wanataka. Naunga mkono kujumuishwa kwa wale walio na tajiriba na ujuzi mbali mbali. Kwa hakika, hapa tutapiga hatua maana katika majadiliano yao, watafika mahali ambapo watatoa uamuzi wa mwisho ulio sawa na ambao hautaleta utata wa aina yoyote. Kwa kumalizia, nitazungumzia swala la maeneo bunge. Tukisema Kwamba kutakuwa na utata kwa sababu ya mazoea, basi ni dhahiri kuwa hakukuwa na haja ya kubadilisha maeneo bunge 212 yafike 290. Ikiwa idadi imezidi, kuna haja ya kugawanya maeneo bunge hayo ili huduma ziwe karibu na mwananchi. Kwa maeneo madogo ya wadi, ikiwa wadi moja iliyo na wapigaji kura 70,000 itaongozwa na Mbunge wa Kaunti mmoja ni shida. Ni dhahiri kwamba itastahili igawanywe ndio huduma ziweze kumfikia mwananchi pale chini aliko. Kwa hivyo, rai yangu ni kwamba kuna haja ya kuangalia swala la mipaka. Tumekumbwa na janga Magarini, ikizingatiwa kuwa eneo moja kiutawala liko katika eneo bunge lingine. Eneo hilo hilo liko katika wilaya nyingine. Kwa mfano, eneo la Shakahola. Tulitoa taarifa kwamba kuna jambo ambalo haliendi vizuri huko lakini kwa sababu liko katika eneo bunge la Magarini, na eneo lenyewe liko katika wilaya ya Malindi kiutawala, jambo hilo halikuweza kushughulikiwa. Hakika, madhara tuliyopata yalikuwa ya kutamausha hapa nchini Kenya na ulimwengu mzima. Hivyo basi, napendekeza kuwa wakati tume hii itaanza kugawanya maeneo bunge, ihakikishe kuwa sehemu za maeneo bunge haya hazipatikani kiutawala katika maeneo mengine; yote yawe upande mmoja. Nikichukua mfano wa maeneo bunge ya Magarini na Malindi, yamegawanywa na mto. Hata hivyo, kuna mahali ambapo tarafa moja imegawanywa na mto na ipo upande wa Malindi na vile vile upande wa Magarini. Ukifika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}