GET /api/v0.1/hansard/entries/1407795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1407795,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1407795/?format=api",
"text_counter": 374,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, naunga mkono Seneta wa Kaunti ya Narok. Kuna mambo ambayo yanafaa kuangaliwa. Kenya ina kaunti 47 na kila mojawapo ina shida zake. Katika ulimwengu huu, miti haitoshani. Magavana walipochaguliwa katika kipindi cha kwanza na cha pili, waliajiri wafanyikazi waliokuwa na uhusiano nao. Wengine walikuwa wezi na walaghai. Magavana waliochaguliwa 2022 wanajaribu kusaidia ugatuzi. Watu wanafaa kulipwa madeni. Tunajua kaunti nyingi zina madeni. Kwa mfano, Kaunti ya Embu ina madeni ya bilioni Kshs2.2. Kitu kingine in wage bill . Naomba Maseneta wenzangu tusaidie kuendeleza ugatuzi kwa kuangalia usimamizi wa kazi katika kaunti zetu. Kuna kaunti ambazo zimepewa mabilioni ya pesa. Kaunti kama vile Turkana imepewa pesa nyingi kuliko Kaunti ya Embu ilhali tunasema magavana wanafaa kufanya kazi. Tunapozungumza kuhusu magavana kulipa pending bills na wage bill, hatuangalii pesa ambazo wanapewa au mishahara ambayo wanalipa. Kule vijijini, watu waliowachagua wanasema kuwa hakuna kazi ambayo wanafanya. Ni muhimu tujue ili tusionekane kuwa hatuelewi kama Maseneta. Tulikuwa tunapigia upato mfumo wa kura moja, mtu mmoja, shilingi moja. Tulipoingia katika Bunge hili, magavana walitaka pesa za kaunti ziwe bilioni Kshs425 lakini tukawapa bilioni Kshs415. Kwa sababu ya shida ya ukosefu wa pesa iliyokuwa wakati Serikali ya Kenya Kwanza ilipoingia mamlakani, tuliwapa bilioni Kshs385. Hapo"
}