GET /api/v0.1/hansard/entries/1407797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1407797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1407797/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ndipo makosa yalifanyika. Hatukufikiria sababu ambazo magavana ambao ni wasomi walikuwa nazo wakati walipoitisha pesa hizo. Ni lazima tuangazie mambo ya pending bills na wage bill . Sio lazima iwe vita kila wakati. Ndio maana tumepitisha kuwa wapewe Kshs415 billion. The Salaries and Remuneration Commission (SRC) imependekeza wapewe Kshs405 billion. Tunataka kuona kama watafanya hiyo kazi yote tukiwaongezea pesa. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, naunga mkono lakini kuna mambo ambayo lazima tuangalie hata kama pesa inakuliwa. Tunafaa kujiuliza kwa nini magavana wanaitisha pesa nyingi. Ni kwa sababu kuna shida katika kaunti zetu. Kuna mambo wanayofaa kutekeleza lakini pesa haitoshi. Watu wanaendelea kufanya miradi ya maji na mambo mengine. Juzi madaktari walipogoma, watu walianza kusema kuwa kuna ubadhirifu wa pesa. Walisahau kuwa mambo ya afya yamegatuliwa. Shida kama hizo zinatokea kwa wingi. Magavana wana ujuzi ya kufanya kazi lakini bajeti zao hazilingani na pesa tunazowapa. Naomba sisi Maseneta tuangalie jinsi mambo yalivyo bila kusisitiza kuwa kuna ubadhirifu wa pesa ilhali tunataka walipe madeni. Kwa mfano, Kaunti ya Embu ina madeni ya bilioni Kshs2.2. Gavana atalipaje madeni ikiwa hana pesa ya kulipa mishahara? Kuna watu waliokuwa wanapata mishahara lakini hawapokei. Watalipa mishahara na nini? Wakati umefika wa magavana kulainisha kaunti zao. Bw. Naibu Spika, naunga mkono Hoja hii. Tunafaa kuzingatia mfumo wa mtu mmoja, kura moja, shilingi moja."
}