GET /api/v0.1/hansard/entries/1407856/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1407856,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1407856/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi nitoe maoni yangu kuhusu Mswada huu ambao ni sheria mpya inayoletwa na Seneta Beatrice Ogola. Namshukuru sana kwa sababu katika sheria hii, ataweka jina lake katika maktaba ya Seneti, Bunge na Kenya mzima miaka itakayokuja kwamba alipitisha sheria ambayo ilipatia kinga ya kutosha kwa akina mama na watoto wanaokuja katika inchi hii ya Kenya. Ningependa sana kumpatia motisha kwamba kazi nyingi tunazofanya hapa Seneti zitasahaulika, ila, sheria inayopitishwa hapa Bungeni katika nakala za Seneti na wakenya wazima, watakumbuka miaka yote. Kwa hivyo, najua amefanya kazi nyingi ila nampa moyo aendelee vivyo hivyo, na ikiwezekana alete sheria zingine ambazo zitasaidia. Kwanza Bi Spika wa Muda, nasema pole sana kwa wale waliopoteza maisha yao katika mkasa tuliopata Tana River. Wengi wa waliokufa katika mashua ile ni kina mama na watoto. Walikuwa wanavuka kutoka Madogo kuelekea Garissa kwa kazi zao za kawaida. Bi. Spika wa Muda, majanga au shida zikitokea, wanaoumia zaidi ni kina mama na watoto. Mswada huu una vipengele ambavyo vitatoa nafasi ya kutunza watoto wanaozaliwa pamoja na kina mama wajawazito. Huu ni Mswada muhimu hapa Kenya. Wiki hii tulikuwa kule Tana River pamoja na viongozi wa Serikali kuangalia hali ya mafuriko. Tuliona shida kubwa ambayo wananchi wanapata. Wananchi hawana chakula cha kutosha, wanaumia, kuna mbu usiku na hali ya usalama ya imeharibika. Watu wametoka kwa nyumba zao ambazo zimesombwa na maji na sasa wako barabarani. Shughuli za kutafuta riziki ya kila siku zimeharibika. Kwa hivyo, watu wanaumia. Usalama vile vile umezorota kwa sababu watu wanafanya uhalifu kupata jinsi ya kujikimu. Kina mama wajawazito wanapata shida zaidi. Tulipokwenda kule, kulikuwa na watoto wadogo ambao mimi nilishindwa tutafanya namna gani licha ya kuwa tulikuwa tumewapelekea chakula. Sisi kama wazazi ambao tumepita hiyo stage tunajua kuwa watoto lazima wawe na nguo za kutosha na mahali pazuri pa kulala. Watoto kama hao hawafai kulala nje kwa sababu usiku baridi huwa kali kule Tana River. Ni watoto wanaotaka lishe bora na chanjo. Utapata kuna mama ameshika mtoto ilhali hali yake si sawa kwa sababu anatarajia mtoto mwingine. Watoto nao pia wana shida. Nina furaha kwa sababu Mswada huu ukiwa sheria utashurutisha Serikali za kaunti na Serekali ya kitaifa kuhakikisha kwamba kina mama wanapewa nafasi ya kuwatunza watoto wao. Ukienda katika hospitali nyingi, utakuta kuwa hazijawapa kina mama nafasi ya malezi bora ya watoto wao. Mswada huu unapendekeza kwamba waziri wa kaunti ashurutishwe kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kina mama na watoto wanapata huduma za kiafya nzuri katika hospitali zetu. Kule kwetu Tana River, mbali na zile shida tulizonazo kwa sababu ya mafuriko, kwa kawaida, kina mama wetu wanapata shida sana wakati wanapokwenda kujifungua. Wengi wao hawapati nafasi ya kutembelea kliniki vile inavyotakikana. Wengi wao pia"
}